MISS TANZANIA GENEVIEV MPANGALA KUANZA KUVUA TAJI KESHO


SHINDANO la kumtafuta mrembo wa Chang'ombe kwa mwaka 2011 linatarajia kufanyika Ijumaa hii yaani Juni 17 katika ukumbi wa Tcc Club Jijini Dar es Salaam huku shindano hilo likisindikizwa na bendi ya Mapacha watatu watakaoanza burudani kuanzia saa 2 usiku.

Akizungumza jijini Dar es Salaam mratibu wa Shindano hilo ambaye pia mwalimu wa warembo hao Stela Solomon amesema kuwa maandalizi yote ya shindano hilo yamekamilika kinachosubiriwa kwa sasa ni warembo hao 12 kupanda jukwaani kuchuana vikali kwa lengo la kuwania taji hilo la changombe linaloshikiliwa na Miss Tanzania 2010 Genevive Emanuel Mpangala.

Stela amesema kuwa warembo hao ambao wamekuwa kambini katika heteli ya National kwa wiki tatu sasa wamekuwa na hamasa kubwa miongoni mwao kutoakana na changamoto iliyoko mbele yao ya kuhakikisha kuwa wanarith mikoba ya Genevive na hii inatokana na mnyange huyo wa Tanzania kufika mara kwa mara kwenye kambi hiyo na kuweza kuwafunda warembo hao.

'Kwa kweli inapendeza sana kuona miss Tanzania mara kwa mara yupo na waerembo hao huku akitambua kuwa ndipo alipotoka kwa hiyo washiriki wa shindano la mwaka huu kila mmoja ameahidi kufanya vema hivyo nampongeza sana mtoto huyo wa kiongozi wa zamani wa Yanya Emanuel Mpangala' alisema Stela

Amesema kuwa mshindi wa kwanza katika kinyang'anyiro hicho atajinyakulia kitita cha shilingi laki sita, wapili laki tatu, watatu laki mbili wann na watano kila mmoja laki moja na nusu na wengine saba waliobaki kila mmoja ataondoka na kitita cha shilingi laki moja.
Washiriki wa shindano hilo ni Salma Leonald, Ummy Mohamed, Sasha Seith, Iren Jackson, RoseMary Osward,Sarah Paul, Joyce Maweda, Sanza Kajubi, Husna Twalib,Elizabeth Boniface,Winfrida Kaba na Cyntia Kimasha.
Shindano hilo limedhaminiwa na Papazii Entertainment, Voda Com, Redds,Times Fm,Paris Pub,ZH Pope,Zizzou Fassion,Ben Expedition, Screen Masters,Fredutor Entertainment,Chef Pride na Travel Patner.

Comments