MISS TABATA 2011 NI FAIZA ALLY



KIMWANA Faiza Ally (19), usiku wa kuamkia jana alitangazwa rasmi kuwa malkia mpya wa taji la 'Miss Tabata 2011' baada ya kuwabwaga warembo wengine 20 katika shindano lililoweka rekodi ya pekee kwa aina yake kutokana na kushuhudiwa na umati mkubwa wa wapenzi wa sanaa ya urembo kwenye ukumbi wa Dar West Park, Tabata.

Ushindi wake mbali na kumpa tiketi ya kushiriki shindano la Miss Ilala pia alikwenda nyumbani na zawadi ya shilingi milioni 1.
Godliver Mashamba (22), alinyakua shilingi 500,000 baada ya kuibuka nafasi ya pili, wakati mrembo Lilian Bryson (22) alizawadiwa shilingi 300,000 baada ya kushika nafasi ya tatu.
Kimwana Rita Mvungi (21), alishika nafasi ya nne, wakati Agustina Mshanga (20) alikamata nafasi ya tano--na kila mmoja kuondoka na shilingi 200,000.
Warembo wengine watano waliokamilisha 10-bora ya Miss Tabata mwaka huu na kuzawadiwa 100,000 kila mmoja ni Nasra Salim (21), Willieth Wilson (22), Prisila Mchemwa (19), Crecensia Haule (20) na Edina Mnada (21). Warembo 10-bora ndio watakaoiwakilisha Tabata katika kinyang'anyiro cha Miss Ilala baadaye mwaka huu.

Comments