MISS DAR INTER COLLEGE KUANZA KUJINOA JUMAPILI

WAREMBO 15 wanaotarajiwa kushiriki shindano la Miss Dar Inter college mwaka 2011 wataanza rasmi mazoezi ya kujiandaa na shindano hilo jumapili hii kwenye ukumbi wa Break Point ulipo katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Mratibu wa shindano hilo Vicky Kimaro alisema warembo hao watakaotoka katika vyuo vya Cbe, IFM, Ustawi wa Jamii na DSj watakuwa chini ya ukufunzi wa Beatrice Lukindo na mrembo anayeshikilia taji hilo, Rose John.
Alisema maandalizui mengfine kwa ajili ya shindano hilo yanaendelea ikiwamo kusaka wadhamini watakaiosaidia kufanikisha shindano hilo linalohusisha wanafunzi kutoka vyuo vya elimu ya juu vya jiji la Dar es Salaam.
Aliongeza kuwa mwaka huu wamejipanga kuhakikisha wanapata washiriki bomba ambao wataiwakilisha vema kitongoji hicho katika ngazi inayofuata na hatimaye fainali za Miss Tanzania, huku tarehe ya shindano hilo itatangazwa baadaaye.
"Ndio maandalizi yameanza, nafasi zipo wazi kwahiriki wenye sifa kujitokjeza katika shindano letu, pia tunaomba makamopuni mbalimbali yajitokeze kushiriki shindano kletu", Alisema Vicky.

Comments