MIMI NA H-BABA NI RAHA TUPU


NYOTA wa filamu nchini Frola Mvungi amesema anafurahia maisha yake ya uchumba na mwanamuziki wa muziki wa bongo fleva nchini Hamis Ramadhan Baba ‘H- Baba’ tofauti na watu wanavyodhani.
Flara amesema hiyo inatokana na kumwelewa na kumsapoti kazi zake tofauti na wapenzi wake aliowahi kuwa na uhusiano nao hapo awali.
“Ni mara chache sana mtu asiye msanii kukuelewa jinsi ya utendaji wa kazi zako,  nafurahia maisha na mchumba wangu H. Baba kwa sababu yeye ni msanii na mimi ni msanii kwa hiyo hana mashaka na mimi wala mimi sina mashaka naye wote tunaelewana,”Alisema
Alisema unapokuwa na mahusiano na mtu asiye msanii ni vigumu sana kukuelewa hasa pale unapotingwa na masuala ya upigaji picha ama  kuchelewa kurudi nyumbani ni lazima mgombane kwani anakuwa hafahamu mazingira ya kazi hizo.
Frola amewahi kushiriki katika filamu kadhaa ambazo zimeweza kushika ilivyo zikiwemo Young Billionaire,September 11,  Handsome wa kijini na nyinginezo huku akishirikiana na H-Baba wamefanikiwa kurekodi filamu mpya inayaojulikana kwa jina la Trafic Pori.

Comments