MARADHI YANAYOTIBIWA NA KITUNGUUMAJI-2




Ukurutu (Eczema):
Chukua juisi ya kitunguu na nanaa (mint) vipimo sawa, tengeneza kama krimu (cream) na ujipake baadae pangusa ukurutu kwa maji ya siki nyepesi, rudia kila siku pamoja na kujiepusha na kila kinachochea hisia. Kula matunda, mboga na asali kwa wingi.

Saratani ya ngozi:
Chukua juisi ya kitunguu maji, uwatu uliosagwa na salfa manjano kiasi cha robo kijiko kidogo; tengeneza marhamu jipake kila siku. Baada ya kuosha jioni jipake mafuta ya zetuni endelea hivyo kwa muda wa wiki.
Mgonjwa wa figo na vijiwe:
Chukua kitunguu bila kukichambua, tia mbegu ya tende baada ya kuichoma kama vile buni na kuisaga; halafu kila siku kula kimoja kula kimoja kwa muda wa wiki.
Kikohozi kwa wakubwa na wadogo:
Saga kitunguu kitie ndani ya kikombe cha asali; iwache kwa muda wa masaa matatu (3) kisha uisafishe. Kula kiasi cha kijiko kimoja kila baada ya chakula.
Kisukari (Diabetes):
Kila siku kula kitunguu. Sukari itashuka na baadae kula mzizi wa kabichi (cabbage).

Maradhi ya macho:
Chukua maji ya kitunguu na asali vipimo sawa halafu ujipake jichoni (kama unavyojipaka wanja) , (dawa hii naamini ni dawa bora kwa maradhi ya macho yote nakuambuka marehemu bibi yangu alikuwa akiwatibu wagonjwa wenye mtoto wa jicho kwa kutumia dawa hii) jipakae jichoni kwa kutumia glassrod au kama huna kifaa hicho unaweza kutumia nyoya la kuku au ndege yoyote.

Kikohozi:
Chemsha maji ya kitunguu maji na asali kunywa kijiko kimoja kila baada ya kula na weka kibandiko cha kitunguu maji juu ya kifua na majani yake kwa bendeji kabla ya kulala.

Kufungua choo:
Chambua kitunguu, tia katika maziwa na kunywa.
Kutia nguvu na nishati:
Choma kitunguu pamoja na maganda yake halafu kichambue na ukikande katika asali na samli, weka katika mkate wa ngano nzima kama vile sandwich. Kula wakati wa chakula cha asubuhi na unywe maziwa nusu lita.

Kupunguza uzito:
Kwa anaetaka kufurahi mwili wake uwe mzuri na mwepesi, kuyayusha mafuta na kuondoa kitambi na mwili tepwetepwe miongoni mwa wanaume na wanawake basi afwate hivi:
1. Kila siku kunywa maji ya kitunguu maji kiasi cha kijiko kimoja kidogo unaweza kuchanganya katika juisi ya matunda ukanywa.
2. Soma sana katika masaa ya mwisho wa usiku na kukizingatia ukisomacho (ukisoma Quraan utapata faida 2 kwa wakati mmoja, moja ya hapa duniani na moja ya huko tunapokwenda akhera) pia usile chakula cha usiku isipokuwa maziwa ya mgando kikombe kimoja, au matunda.
3. Tembea sana na kufanya mazoezi kwa wingi.
Inshallah leo nitakomea hapa. Mola atujaalie afya njema. Amin

Comments