MAPACHA WATATU, AKUDO IMPACT JUKWAA MOJA JULAI 2


KUNDI la mapacha watatu pamoja na bendi ya Akudo Impact watafanya onyesho la pamoja siku ya Julai 2 kwenye ukumbi wa Vatican City uliopo, Sinza jijini DAr es Salaam.
Onyesho hilo limeandaliwa na kampuni ya kampuni ya Big One Entertainment Company Limited chini ya Mkurugenzi wake Aboubakar Mwanamboka lina lengo la kutoa burudani pamoja na kuonysha ushirikiano baina ya wasanii wa dansi.
"Mara nyingi imezoeleka kuwa bendi za dansi haziwezi kutumbuiza katika jukwaa moja kutokana na bifu walizonazo, sisi tunataka kuondoa dhima hii", Amesema Mwanamboka.
Pamoja na hilo, Mwanamboka amesema kuwa kampuni yake imejipanga kuandaa matamasha mengi ya muziki wa dansi ili kuhakikisha mashabiki wanapata burudani ya kutosha.

Comments