MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA SHEREHE ZA MAADHIMISH​O YA SIKU YA MAZINGIRA, SONGEA

16:- Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akibonyeza kitufe kuashiria kuzindua rasmi maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani yanayofanyika kitaifa mjini Songea mkoani Ruvuma. Sherehe hizo zimeanza leo Juni 01, katika Uwanja wa Majimaji. Kulia ni Mke wa Makamu wa Rais Mama Zakia Bilal na (katikati) ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Dkt. Christine Ishengoma. 
13:- Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, DKt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kikosi cha kuzuia ujangili Kanda ya Kusini, Metson Mwakanyamale (kushoto) kuhusu ufugaji wa Mamba, wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya maonyesho katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, zilizozinduliwa leo Juni 01 kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea Mkoa wa Ruvuma. Kulia ni mkewe Mama Zakia Bilal.


10:- Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, DKt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma ujumbe kuhusu zoezi la kuzuia uchomaji wa misitu katika mabango yaliyokuwa yameshikwa na vijana, wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya maonyesho katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, zilizozinduliwa leo Juni 01 kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea Mkoa wa Ruvuma. Kulia ni mkewe Mama Zakia Bilal.

 Makamu akisalimiana na madiwani wa Manispaa ya Songea baada ya kuwasili.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia ngoma ya asli baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Mkoani Ruvuma leo Juni 01, kwa ajili ya kuzindua sherehe za maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Majimaji, mjini Songea Mkoa wa Ruvuma.
 Makamu Dkt Bilal, akisalimiana na Madiwania wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Vijijini, baada ya kuwasili. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa zinduzi wa Sherehe za maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani, zinazofanyika kitaifa mjini Songea Mkoani Ruvuma. Picha zote na  Muhidin Sufiani-OMR .

Comments