MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AKUTANA NA BAN KI MOON, AUNGURUMA JIJINI NEW YORK KATIKA MKUTANO WA UMOJA WA MATAIFA KUHUSU UGONJWA WA UKIMWI

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ugonjwa wa Ukimwi, unaoendelea jijini New York.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Ban Ki Moon, wakati alipokutana naye kwa mazungumzo ofisini kwake jijini New York, jana Juni 8, 2011 baada ya kuhudhuria ufunguzi wa mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ugonjwa wa Ukimwi, unaoendelea jijini hapa.
  Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dkt. Asha Rose Migiro, akisalimiana na Naibu waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Maalim, wakati waziri huyo alipoongozana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, katika ofisi ya Umoja wa Mataifa (UN) New York jana Juni 8 kwa ajili ya mazungumzo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ugonjwa wa Ukimwi, unaoendelea jijini New York. Picha zote na Muhidin Sufiani-OMR

Comments