MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AFANYA MAHOJIANO NA MTANGAZAJI WA UN REDIO NEW YORK

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mahojiano na mtangazaji wa Redio ya Umoja wa Mataifa (UN), Flora Nducha, muda mfupi baada ya kuhudhuria mkutano wa majadiliano kuhusu masuala ya ukimwi ulioandaliwa na Umoja wa Mataifa unaofanyika jijini New York,  Juni 10, 2011, jijini New York.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilala, akisalimiana na mtangazaji wa Redio ya Umoja wa Mataifa (UN) Flora Nducha, wakati mtangazaji huyo alipofika kwa ajili ya kufanya mahojiano naye  kuhusu maudhui ya mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ukimwi uliofanyika jijini New York, na unatarajiwa kumalizika Juni 10, 2011.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa na baadhi ya viongozi wenzake kutoka nchi mbalimbali wakati akishiriki mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ukimwi unaofanyikajijini New York jana.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na mshauri Mkuu wa ufundi na Asasi ya Viongozi wa Afrika inayohusika na vita dhidi ya Malaria, Dkt. Melanie Renshaw (wa pili kulia) na Balozi wa Tanzania wa Umoja wa Mataifa, Ombeni Sefue (kulia) na Mkurugenzi wa Sekretarieti ya Umoja wa Mataifa inayohusika na vita dhidi ya Malaria, Saleemah Abdul-Ghafur  (kushoto), wakati walipomtembelea Makamu wa rais jijini New York Juni 9 na kufanya mazungumzo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Tacaids, Dkt. Fatma Mrisho (kushoto) na Mkurugenzi wa Tume ya Ukimwi Zanzibar, Dkt. Omari Shauri (kulia) wakati walipomtembelea Makamu wa rais jijini New York Juni 9 na kufanya mazungumzo. Picha zote na Muhidin Sufiani-OMR

Comments