MAASKOFU WAMPA SAA 48 RAIS JAKAYA KIKWETE KUWATAJA VIONGOZI WAUZA UNGA VINGINEVYO...

Wananchi  wa Mbinga wakimsalimia kwa shauku Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya kumalizika ibada ya Kumsimika na kuwekwa wakfu kwa Askofu Mpya wa jimbo Katoliki Mbinga,Mhashamu John Ndimbo zilizofanyika katika  kanisa la Mtakatifu Kilian mjini wa Mbinga, mkoani Ruvuma jana(picha na Freddy Maro).


Na Datus Boniface


MAASKOFU wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), wamempa Rais Kikwete saa 48 kuanzia sasa kuwataja kwa majina viongozi wote wa dini anaowatuhumu kuuza unga.
Endapo Rais Kikwete akishindwa kuorodhesha majina yao ni wazi kwamba ataonekana sio mkweli na wataamua la kufanya (hawakutaja).
Rais Kikwete alitoa kauli hiyo juzi alipokuwa akihutubia waumini wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mbinga wakati wa ibada maalumu ya kupewa daraja la uaskofu na kusimikwa kwa askofu wa jimbo hilo, Mhashamu John Ndimbo, katika kanisa la kiaskofu la Mtakatifu Killian iliyohudhuriwa pia na Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamini Mkapa.
Alisema baadhi ya viongozi hao wamekuwa wakishiriki kufanya biashara hiyo ya dawa za kulevya kwa kuwatumia vijana ambao huwafanyia mipango ya kuwatafutia hati za kusafiria (Passport) kwenda nchi za nje.
Badala yake Rais Kikwete amewataka viongozi hao nchini kuikemea biashara hiyo na kujenga uhusiano mzuri na vyombo vya dola katika kuhakikisha biashara hiyo inakomeshwa kwa kuwafichua wahusika wanaoifanya ili wachukuliwe hatua za kisheria.
Agizo la CCT lilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wake taifa, Askofu Peter Kitula katika mkutano wake waandishi wa habari.
“Tunampa siku 48 rais awataje kwa majina viongozi hao ambao yeye anadai wanajihusisha na kuuza dawa na kama atashindwa kufanya hivyo tunamtafsiri ni mwongo na mzushi” alisema Kaimu Mwenyekiti wa CCT…..
Tunasikitishwa na kushangazwa kwa kauli hiyo na tunamheshimu kama kiongozi wa nchi, hivyo tunampa saa hayo awataje kwa majina” alisema Kaimu Mwenyekiti Askofu Mokiwa wakati akichangia hoja ya Mwenyekiti.Katika mkutano wao, walisema kama Rais anawafahamu viongozi wa dini wanaohusika na biashara ya kuuza unga iweje anashindwa kuwachukulia hatua za keshiria ikiwemo kuwakamata na kufunguliwa mashitaka.
Walisema viongozi wa dini wanajukumu la kutetea na haki mbalimbali za wananchi, na kuionya serikali pale inapokosea. Hivyo kauli ya Rais Kikwete haina ukweli wowote.
Rais Kikwete katika ibada hiyo alikaririwa akisikitika kutokana na watumishi hao kujiingiza katika biashara hiyo badala ya kukemea matumizi yake.
“Inasikitisha sana na kutisha, biashara hii haramu sasa inawavutia hata watumishi wa Mungu, taifa letu litaharibika tusipokuwa makini katika hili kwani baadhi yenu tumewakamata.
“Kwa kauli zenu kemeeni jambo hili kwa kuelimisha jamii hususan vijana waweze kuepuka na matumizi ya dawa hizi,” alikaririwa Rais Kikwete.

Comments