LUNDENGA NA KAMATI YAKE KUWAFUNDA WASHIRIKI MISS TABATA KESHO


                                Washiriki wa Miss Tabata wakiwa Mikumi

Kamati ya Miss Tanzania kesho itatembelea kambi ya Miss Tabata iliyopo Da’ West Park , Tabata.
Kamati hiyo ikiongozwa na Mratibu wa Vodacom Miss Tanzania Hashim Lundenga itawafunda warembo hao kabla ya kushiriki kwenye kinyang’anyiro hicho siku ya Ijumaa.
“Tutaongea nao ili kujua uwezo wao kabla hawajapanda jukwaani kushindania taji. Pia tutawapa vidokezo vya urembo,” Lundenga alisema.
Warembo 22 watashiriki kwenye kinyang’anyiro hicho ambapo bendi maarufu nchini African Stars “Twanga Pepeta” itatumbuiza kwenye shindano hilo ambalo ni kivutio cha wengi jijini.
Wiki iliyopita warembo hao walitembelea Mbuga ya Wanyama ya Mikumi iliyoko Mkoani Morogoro. “Lengo la ziara hiyo ilikuwa ni kutangaza utalii wa ndani. Warembo walipata nafasi ya kuwaona wanyama waishio kwenye mbuga hiyo. Pia walijifunza mambo mengi ikiwemo kujua tabia za wanyama na ndege wote waliishio katika mbuga hiyo,” alisema mratibu wa shindano hiyo Joseph Kapinga.
Warembo waliosafiri na ambao watashiriki ni Marion Augustino (19), Neema Marwa (18), Catherine Julius (20), Lilian William (20), Godliver Mashamba (22) na Dorice Mutabingwa (21).
Wengine ni Sweetlily Suleiman (21), Maria John (21), Happyness Emmanuel (18), Cresensia Haule (20), Mariam Manyanya (21), Agustina Mshanga (20), Nasra Salim (21), Faiza Ally (19) na Edina Mnada (21).
Pia wamo Angela Fortunatus (21), Lucia Joseph (20), Lilian Brayson (22), Rita Mvungi (21) na Willieth Wilson (22).
Miss Tabata 2011 imedhaminiwa na Dodoma Wine, Vodacom, Redds Original, Integrated Communications, Paris Pub, Fabak Fashion, Freditto Entertainment, Chicken Hut, Travel Partners, Ben Expedition, Screen Masters, Sean Entertainment, Michuzi blogspot, Anech Stationary na Vayle Springs
Consolata Lukosi ndiye mrembo anayeshikilia taji la Miss Tabata.
Mrembo huyo alikuwa nambari tatu mwaka jana kwenye shindano la taifa Vodacom Miss Tanzania kabla ya kushinda taji la Redds Ambassador.
Mashindano hayo ya urembo yanaandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts.

Comments