LUNDENGA AWAONYA WASHIRIKI MISS DAR INTER COLLEGE 2011

 MRATIBU wa Miss Tanzania Hashim Lundenga akizungumza na warembo wa Miss Dar Inter College, kushoto ni mrembo anayeshikilia taji Genevieve Mpangala na kulia ni mkuu wa Itifaki wa Miss Tanzania, Albert Makoye.

WAREMBO wanaoshiriki shindano la kumsdaka miss Dar Intercollege wameonywa kuzingatia zauidi elimu kwani ndiyo msingi wa maisha yao.
HAyo yalisenmwa jana na mkurugenzi wa kampuni ya Lino International Agency inayoandaa shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga alipotembelea kambi ya warembo hao iliyopo katika ukumbi wa Brake Point, jijini Dar es Salaam.
Amesema pamoja na kushiriki masuala ya urembo hawana budi kufuatilia masomo yao na kufanya urembo kama sehemu ya maisha yao.
"Nafahamu kama ninyi ni wanafunzi,. hivyo msijisahau kufuatilia masomo na kuendekeza masuala fulani ambayo hayatawasaidia katika jamii kwa sabau ya urembo, fanyeni urembo na kisha muendelee na masomo yenu", Alisema.
Shindano hilo litafanyika kesho katika ukumbi wa Sunciro, Sinza jijini Dar es Salaam ambapo msanii wa bongofleva Dully Sykes atapamba onyesho hilo.

Comments