KUMEKUCHA MISS SINZA 2011

AMISUU MALIKI, MISS SINZA 2011

NA MWANDISHI WETU
WAREMBO wanaowania taji la Miss Sinza 2011, mwishoni mwa wiki iliyopita,
wameshiriki katika michezo mbalimbali kwenye Ufukwe wa Mikadi, uliopo Kigamboni,
jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya shindano lao.
Kinyang’anyiro cha Miss Sinza, kinatarajiwa kufanyika Juni 24, mwaka huu kwenye
Ukumbi wa Vatican, jijini, ambapo jumla ya warembo 15 watapanda jukwaani siku
hiyo kuwania taji linaloshikiliwa na Amisuu Malick.
Michezo walioshiriki warembo hao, ilikuwa ni soka, ‘rede’, kukimbia pamoja na
kuogeleaji, ambapo walionyesha umahiri mkubwa, huku wakishuhudiwa na wakufunzi
wao, Amisuu na Salma Ali, pamoja na mwalimu wa shoo, Omari Musa ‘Bokilo’.
Wakizungumza wakati wa tukio hilo, warembo hao walionyesha kufurahia michezo
hiyo, wakiwapongeza waandaaji kwa hilo.
Akizungumza wakati wa nichezo hiyo, mwandaaji wa shindano hilo, Titina
Makutikaalisema kuwa wameamua kufanya tukio hilo, ili kuanza kuangalia uelekeo
wa warembo wao katika suala la michezo ambalo ni moja ya kipengele
kinachoshindaniwa katika fainali za Dunia, Miss World.
Alisema kuwa pia mazoezi hayo, yalilenga katika kuwajenga zaidi warembo hao
waweze kuwa wepesi katika kufuata na kushiriki katika maandalizi ya
kinyang’anyiro hicho kinachotarajiwa kuwa cha aina yake.
“Warembo wetu bado wanaendelea na maandalizi yanayofanyika katika ukumbi wa
Vatican kila siku ambapo maendeleo yameonekana kuwa mazuri hali inayotupa
matumaini ya shoo yetu kuwa ya aina yake, alisema.
Alisema kuwa kutokana na ubora wa warembo wao, wanaamini taji la Miss Kinondoni
litatua Sinza, kabla ya baadaye mmoja wa warembo wao kufanya kweli katika
fainali za Miss Tanzania kuwania taji linaloshikiliwa na Genevieve Emmanuel
kutoka Temeke.

Comments