KOCHA SIMBA AIMARISHA UKUTA WAKE, TAYARI KUWAVAA DC MOTEMA PEMBE J'2

KOCHA wa timu ya soka ya Simba Mganda Moses Basena amesema amefanyia kazi udhoofu uliokuwepo katika safu ya ulinzi ya kikosi hicho hali inayosababisha timu hiyo kufungwa katika michezo yake.
Kwa sasa kikosi cha timu hicho kipi kambini jijini Tanga kikijiandaa na mechi ya kuwania kuingia nane bora ya kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya DC Motema Pembe ya Jamhuri ya Kidem,okrasia ya Congo jumapili hii katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Comments