KIPA MKENYA ATUA SIMBA, TIMU KUTOVUNJA KAMBI

WAKATI kipa kutoka nchini Wills Ochieng akiwasili leo kwa ajili ya kujaribiwa katika klabu ya soka ya Simba, wapinzani wake katika mechi ya kwanza kuwania ubingwa shirikisho, timu ya DC Motema Pembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wanatarajiwa kuawsili kesho.

Mechi hiyo inatarajiwa kupigwa jumapili ya juni 12 kuanzia saa 9.30 alasiri katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Makamu mwenyekiti wa Simba Geofref Nyange ‘Kaburu’ aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kwamba maandalizi kwa ajili ya mechi hiyo yanakwenda vizuri.
“Maandalizi yanakwenda vena na hasa ikizingatiwa wachezaji wetu karibu wote wapo kambini isipokuwa Jerry Santo ambaye alikuwa kwao Kenya kuitumikia timu ya Taifa, tunatarajia awasili leo (jana),” alisema.
Kaburu aliongeza kuwa, kikosi chao hakitavunja kambi baada ya mechi yake ya marudiano dhidi ya Motema Pembe utakaopigwa kati ya juni 19 huko Kinshasa, DRC kwani baada ya mechi hiyo watakuwa wanashiriki michuano ya Kombe la Kagame inayoratajiwa kuanza Juni 21, Dar es Salaam.

Comments