KINO WAVULIWA UBINGWA COPA COCA COLA

MABINGWA watetezi wa mashindano ya Copa Coca Cola, Kinondoni wameshindwa kutetea ubingwa wao baada ya kutolewa na timu ya Temeke kwa mikwaju ya penalti 4-2 kwenye mchezo wa robo fainali uliofanyika kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa, timu hizo zilijikuta zikimaliza kwa suluhu ndipo mshindi alipotafutwa kwa changamoto ya mikwaju ya penalti.
Timu ya Temeke ilikuwa makini zaidi kwenye kipengele hicho baada ya wapigaji wake Rehani Kibingu, Abbasi Kapombe, Gharidi Salum na Masudi Ally kufunga penalti zao.
Wakati Kinondoni wenyewe walipata penalti mbili kupitia kwa Reyna Mgungila na Jumanne Goha huku Yasini Amiri na Mohamed Hussein wakikosa kwa upande wa mabingwa.

Comments