HUYU NDIYE WORGU ALIYETANDIKWA BAKORA 40


SIDHANI kama kipo kitu kikubwa kinachowakimbizia wachezaji wengi wa Afrika kwenda kucheza Ulaya zaidi ya malsahi. Ndio, wapo wengine wanapenda tu kuishi Ulaya, ila wengi wao wanafuata fedha Ulaya na wanapomaliza maisha yao ya mpira hurejea nyumbani.
Nyota wengi wa Nigeria kama akina Daniel Amokachi, Rashid Yekini, Jay Jay Okocha ambao waliwika Ulayam, kwa sas wanaishi na familia zao nchini mwao baada ya kustaafu soka. Zaidi ni fedha nzuri ndio inawapeleka wachezaji wa Afrika Ulaya, hivyo wakati mwingine yanapopatikana maslahi mazuri kwa timu za Afrika, wachezaji huamua kucheza nyumbani, ingawa ni ukweli usopingika, kucheza Ulaya kuna hadhi yake na si kwa Waafrika tu, bali hata kwa waamerika na Waasia.
Akiwa Enyimba ya Nigeria mwaka 2008 baada ya kung’ara na kuwa mfungaji bora wa Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mabao yake 13, na kuiwezesha timu hiyo kufika Nusu Fainali ya michuano hiyo, hayo yakiwa mafanikio makubwa zaidi kwa klabu hiyo tangu itwae ubingwa wa michuano hiyo mwaka 2004, timu nyingi za Ulaya zilianza kummezea mate na akaitwa Ufaransa na Scotland, lakini hakwenda.
Makala moja yenye kichwa cha habari; “Stephen Worgu: The Next African-European Star” iliandikwa kwenye jaridfa la Kick Off la Afrika Kusini, kufuatia mafanikio yake hayo, lakini leo ikiwa ni miaka mitatu baadaye, mshambuliaji yungali Afrika, ila analipwa fedha nyingi, hadi zinamtia wazimu na kuvunja sheria za nchi ya Sudan.
Worgu alijiunga na El- Merreikh ya Sudan msimu wa 2009-2010, akisani mkataba wa miaka minne Oktoba 22 mwaka 2008, ambao kwa Afrika waliwapiku vigogo wa Misri na mabingwa waq kihistoria Afrika, Al-Ahly.
Usajili wa mchezaji huyo, uligharimu si chini ya dola za Kimarekani Milioni 2.5, wakati yeye mwenyewe akipata mshara wa dola za Kimarekani Milioni 1 kwa msimu na kalbu yake ya zamani ikilipwa dola Milioni 1.5.
Alipotua El- Merreikh, Worgu alikabidhjiwa jezi namba 10, tofauti na namba 27 aliyokuwa akiitumia Enyimba, ingawa alianza kwa kusuasua kama Fernando Torres alipotoka Liverpool kuhamia Chelsea.
Akilipwa mshahara mnono na kwa kuwahi kuwa mfungaji wa Ligi ya Mabingwa, matarajio yalikuwa makubwa mno kwa chipukizi huyo wa Nigeria, lakini alicheza mechi sana bila kuziona nyavu ingawa alianza vizuri akiiwezesha Sudan kutetea ubingwa wa Ligi Kuu.
Kwa kuanza kwake na ukame wa mabao, April 21, mwaka 2009, akihojiwa na BBC, Worgu alisema kwamba kilichokuwa kinamsumbua ni kuzoea hali ya Sudean tofauti na nyumbani kwao ambako tamaduni na lugha ziko tofauti kabisa.
“Unaingia uwanjani mashabiki wanaimba jina lako, lakini sielewi wanasema nini hadi inabidi rafiki zangu,”alisema.
Aprili 23, mwaka 2009, akicheza mechi ya kwanza tangu ahojiane na BBC, Worgu alifanikiwa kufunga bao lake la kwanza katika Ligi ya Sudan dhidi ya Al-Ittihad, El-Merreikh ikishinda 2-0.
Licha ya kupewa kadi ya njano mapema kwenye mechi hiyo, Worgu aliwakimbilia mashabiki wa Merreikh kushangilia na kuvua jezi bao lake la kwanza kwenye ligi na kuvua jezi yake, hivyo kuonyeshwa njano ya pili na kuwa nyekundu, ambayo ilikuwa ya kwanza kwenye mashindano hayo.
Baadaye Agosti, Worgu alikutwa anakunywa pombe kitu ambacho ni kosa kwa sheri za Sudan na klabu yake ikalazimika kulipa faini ya pauni Milioni 24, wakati yeye mwenyewe alihukumiwa kupigwa bakora 40.
Septemba 15 mwaka jana 2010, mshambuliaji huyo alijiunga kwa mkopo na Al-Ahly Benghazi ya Libya kabnla ya kurejea Merreikh Juni 15, mwaka huu.
Katika uhamisho huo, mshambuliaji huyo wa zamani wa Enyimba alijiingizia kiasi cha dola za Kimarekani 300,000 wakati Merreikh ililipwa dola 200,000.
Stephen Worgu aliyealiwa Aprili 6, mwaka 1990 mjini Brass, Nigeria, kisoka aliibukia katika klabu ya Ocean Boys F.C. ya kwaio mwaka 2006, msimu ambao aliiwezesha kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya nchi hiyo chi9ni ya kocha wa zamani wa Enyimba International F.C., Maurice Cooreman kabla ya kwenda Enyimba Julai 2007.
Kwa Tanzania, mchezaji huyu alijipatia umaarufu mkubwa 2007 akiwa Enyimba ilipokutana na Simba katika Ligi ya Mabingwa Afrika, hatua ya 16 bora na kumfunga Juma Kaseja mabao sita, Wekundu wa Msimbazi wakitolewa kwa jumla ya 7-1, wakichapwa 4-0 Nigeria na 3-1 Dar es Salaam.
Jumapili akicheza kwa mara ya pili Dar es Salaam na mara ya kwanza kwenye Uwanja wa Taifa, alitokea benchi na kwenda kumfunga Yaw Berko bao ambalo lilikuwa la kusawazisha kwa timu yake, ikitoka 2-2 na mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga.
Wakati anashangilia bao hilo lililoipokonya Yanga tonge mdomoni, ilikuwa ina maana zaidi ya moja. Kufunga bao la kuinusuru timu yake kufungwa katika mechi ya kwanza ya Kombe la Castle Kagame, kufunga bao kwenye mashindano tena dakika chache baada ya kuingia uwanjani, kufunga bao la nne katika ardhi ya Dar es Salaam.
Huyu ndiye Worgu, ambaye pamoja na kucheza kama mshambuliaji pia anacheza nafasi ya kiungo mshambuliaji. Analipwa fedha nyingi japokuwa anacheza Afrika. Kwa sababu Merreikh ni klabu tajiri. Anapendwa sana, yote sababu ya soka yake. Klabu imemlipia faini kubwa kwa kuvunja sheria za Sudan.
WaWorgu, yule Mnigeria aliyeifungia Merreikh bao la kusawazisha ikimeyana na Yanga Jumapili.

Comments