HONGERA JOYCE KIRIA, SASA NI MAMA LINCON


STERINGI wa Bongo Movie Joyce Kiria hivi karibuni amefanikiwa kujifungua salama mtoto wa kiume ambaye amepewa jina la Lincon.
Kiria, ambaye amejipatia umaarufu kupitia uchamguzi wa masuala mbalimbali ya tasnia ya filamu hapa Tanzania kupitia  kipindi hiki cha Bongo Movie kinachorushwa kila jumatano katika kituo cha Televisheni cha EATV,anaendelea salama na kichanga chake hicho.
Pamoja na bongo movie, Joyce pia amejipatia umaarufu kupitia kipindi kinachozungumzia masuala na changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo wanawake kiitwacho ‘Wanawake Live’ ambapo pia hurushwa EATV.
Tunakutakia kila la heri katika makuzi ya mwana,pia mwenyezi mungu bakupe nguvu ili uweze kurejea katika kazi yako ya kuelimisha jamii.

Comments