FREDERICK CHILUBA AFARIKI DUNIA


IMEKUWA ni habari ya kusikitisha Afrika na duniani kwa ujumla baada ya jana kutangazwa kwa kifo cha aliyekuwa rais wa Zambia, Frederick Jacob Titus Chiluba (PICHANI). 
Baada ya kumaliza muhula wake wa uongozi Chiluba alikumbwa na misukosuko mikubwa ikiwamo tuhuma za rushwa.
Kifo cha Chiluba kimetangazwa leo asubuhi na msemaji wake, Emmanuel Mwamba aliyesema kuwa amefariki mida ya saa sita usiku.
Alisema kuwa kabla ya kukumbwa na mauti Chiluba alikuwa hana tatizo lolote lakini alianza kupata matatizo baada ya kuonana na baadhi ya wanasheria wake.
Taarifa ziliendelea kusema kuwa baada ya wanasheria hao kutoka ndipo Chiluba alianza kulia kuumwa na tumbo hadi akakumbwa na mauti na huo ukawa mwisho wa Frederick Chiluba aliyezaliwa Aprili 30, 1943 akiwa rais wa pili wa Zambia kutoka mwaka 1991 hadi 2002.
Chiluba anafariki akiwa ameacha historia ya kuwa Rais wa kwanza wa nchi hiyo kushinda wadhifa huo kwa kutumia mfumo wa demokrasia ya vyama vingi katika uchaguzi uliofanyika mwaka 1991 akiwakilisha Chama Cha Movement for Multiparty Democracy (MMD), akimshinda mpigania uhuru na kiongozi wa muda mrefu wa nchi hiyo, Kenneth Kaunda.
Baada ya kutawala kwa kipindi cha kwanza alichaguliwa kuongoza kwa muhura wa pili mwaka 1996.
Lakini mwaka 2001, alipojaribu kutaka kuwania muhura wa tatu dhidi ya aliyekuwa Makamu wake wa Rais, Levy Mwanawasa aliyesimama kwa Chama cha MMD alimshinda.
Kushindwa kwa Chiluba kulikuwa kama kumemsababishia matatizo kwani alitengenezewa kamati ya kumchunguza kuhusiana na tuhuma za rushwa mwaka 2009.
Kihistoria Chiluba alizaliwa na baba yake aliyejulikana kama Jacob Titus Chiluba Nkonde na mkewe Diana Kaimba na amekulia katika mji wa Kitwe, Zambia.
Chiluba alipofikiasha umri wa kwenda shule alipewa elimu na elimu yake ya sekondari alisomea katika shule ya  Kawambwailiyopo mjini Kawambwa.
Baada ya kumaliza masomo yake ya sekondari na kushindwa alianza kuwa msaidizi wa dereva na baadaye kuwa dereva wa basi.
Kutokana na muonekano wake wa kupendwa na watu aliamua kujiunga na siasa na cheo chake cha kwanza kilikuwa Mkurugenzi wa jiji kabla ya kuwa muhasibu wa Atlas Copco na baadaye aliongezwa cheo na kupelekwa mjini Ndola ambako alianza kujiunga na shughuli za siasa.

Comments