DULLY SYKES KUPAMBA MISS DAR INTER COLLEGE

MKALI wa bongo fleva anayetamba na singo ya Bongofleva Dully Sykes anatarajiwa kupamba onyesho la kumsaka mrembo wa Miss Dar Inter College linalotarajiwa kufanyika juni 17 katika ukumbi wa Club Sunsiro uliopo Sinza, jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Shindano hilo Vicky Kimaro amesema kwamba maandalizi yanaendelea vema na kwamba warembo 15 toka vyuo vya IFM, Ustawi wa Jamii, CBE na DSJ watapanda jukwaani kuwania taji hilo.

Comments