DC MOTEMA PEMBE WATUA JIJINI NA KUSEMA SIMBA SI LOLOTE

KIKOSI CHA DC MOTEMA PEMBE
TIMU ya soka ya Dc Motema Pembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imewasili nioni ya leo tayari kwa mechi yake ya kwanza ya kombe ka shirikisho dhidi ya Simba utakaopigwa keshokutwa  kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza mara baada ya kuwasili, kocha wa timu hiyo Joseph Mukebe alisema kikosi chake kipo vizuri na wamekuja Tanzania kwa ajili ya kushinda si kingine.
Alisema licha ya wapinzani wao kujitapa kuwa watawaadhiri nyumbani, hilo halimtii hofu kwani wameshaiona mapungufu yake na kuyafanyia kazi hivyo itakuwa ngumu kuwafunga.
“Sisi tumekuja Tanzania kwa ajili ya kushinda, hiyo Simba wala haitupi hofu yoyote kwani tunaifahamu vizuri baada ya kuiona katika mechi zake kadhaa na hasa ile ya kuwania ligi ya mabingwa dhidi ya ndugu zetu Tp Mazembe”, Alisema.

Comments