BUNAMWAYA YAFANYA MAUAJI, ULINZI YATULIZWA MOROGORO

BUNAMWAYA ya Uganda imetoa onyo kali katika Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Castle Kagame baada ya kuitandika Elman ya Somalia mabao 4-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mabingwa hao wapya wa Uganda, sasa wanaongoza Kundi B kwa pointi zao tatu na mabao hayo manne, hivyo kuziweka katika wakati mgumu Yanga na El Merreikh zilizopo kwenye kundi hilo, pia ambazo kila moja ina pointi moja.
Mjini Morogoro katika Kundi C, mabingwa wa Kenya Ulinzi walitoka sare ya 1-1 na St George ya Ethiiopia kwenye Uwanja wa Jamhuri.

Comments