ALIYEKUWA KAMANDA WA MKOA WA KILIMANJARO, LUCAS NG'HOBOKO AANGUKA NA KUFARIKI GHAFLA

Na Charles Ndagula, Moshi
MJI wa Moshi na Vitongoji vyake leo  ulilipuka kwa simanzi na majonzi baada ya kudhibitishwa kuwa,aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro(SACP),Lucas Ngh’oboko (pichani) kufariki dunia.
Kamanda Ngh’boko ambaye alikuwa rikizo ya kujiandaa kustaafu mapema mwezi ujao,alifariki ghafla jana asubuhi kaktika Hospital ya Rufaa ya KCMC baada ya kuanguka akiwa mapokezi ya Hospital hiyo.
Kaimu Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro,Yusuph Ilembo,alisema jana kuwa kamanda Ngh’oboko alianguka ghafla Hospitalini hapo ambako alipelekwa kwa ajili ya uchunguzi wa Afya yake.
Baadhi ya askari waliozungumza na waandishi wa habari jana mjini moshi bila kutaja majina yao,wamedai kuguswa na kifo hicho kutokana na kile walichodaia uharaka wa kamanda huyo aliokuwa akiuonyesha kwa asakri wakati wa kutatua matatizo yao.

Comments