YUSUF MLELA NI MTAMU ILE MBAYA-WOLPER

THE Cute wa bongo muvi, Jacqueline Wolper, ameibuka na kufungua moyo wake kuhusu kipaji cha mwigizaji mwenzake, Yussuf Mlela, ambaye amecheza naye picha la Candy, akisema; “Kijana ni mtamu sana”.
Akizungumzia picha picha lao hilo jipya, Jacque alisema kwamba Yussuf Mlela anajua sana kazi na anafahamu vema kuuvaa uhalisia, kiasi kwamba ni mtamu sana kumuangalia anapokuwa anapiga mzigo.
“Kwa kweli tunahitaji waigizaji aina ya Yussuf, kijana anaigiza haswa, tulipokuwa naye location (eneo la kuchezea sinema). Nilikuwa ninampongeza kwa kila scene (kipande) anayocheza, kwa sababu alikuwa anafanya kwa umahiri mkubwa,” alisema Cute huyo.
Katika picha la Candy linalotarajiwa kuanza kupatikana mwishoni mwa mwezi huu mtaani, pamoja na Cute Jacque na ‘The handsome boy’ wa bongo muvi, Yussuf, wakali wengine ni Steven Sandhu, kijana mwingine anayeibuka vizuri kwenye tasniya hiyo.
 

Comments