YANGA WAMWANGUKIA DAVIS MOSHA

MWENYEKITI wa klabu ya soka ya Yanga Lloyd Nchunga amemwangukia aliyekuwa Makamu wake, Davis Mosha (pichani kushoto) baada ya kumteua kuwa mmoja wa Wajumbe wa kamati maalum ya kuchangisha fedha zitakazosaidia kusajili wachezaji wapya itakaowatumia katika msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania bara na michuano ya kimataifa.

Kwa mujibu wa barua hiyo iliyoandikwa na Nchunga kwenda Mosha ya Mei 23 mwaka huu,hafla hiyo inarajiwa kufanyika keshokutwa (jumapili) katika hoteli ya Ragency iliyopo Mikocheni, jijini Dar es Salaam kuanzia saa 12 jioni.

Comments