WATOTO WA JULIO WATOLEWA KILI TAIFA CUP, KAGERA v MBEYA KUKWAANA NUSU FAINALI



TIMU ya soka ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 23 imeyaaga mashindano ya kuwania kombe la Taifa baada ya kufungwa kwa matuta na mkoa wa Kagera katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.
Katika mechi hiyo, timu hixzo zilimaliza dakika 90 kwa sare ya mabao 2-2 hivyo kupelekea hatua ya Penati ambapo Kagera ilishinda kwa 3-1.
Awali ulifanyika mchezo baina ya Mbeya dhidi ya Ruvuma ambapo Mbeya lishinda mabao 3-2.
Kwa mantiki hiyo, Mbeya itakwaana na Kagera katika mchezo wa nusu fainali ya pili utakaopigwa jumatano.

Comments