WATOTO WA JULIO WAANZA VEMA KILI TAIFA CUP KITUO CHA KILIMANJARO

KAIMU MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO,SAID KALEMBO AKIMKABIDHI MCHEZAJI BORA WA MECHI BAINA YA ARUSHA NA TANGA,KIBABU CHANDINGA WA TANGA
KIKOSI CHA TIMU YA VIJANA KIKIOMBA DUA KABLA YA MECHI YAO NA WENYEJI KILIMANJARO

TIMU ya vijana wenye umri chini ya miaka 23 wameanza michuano ya Kili Taifa Cup kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji Kilimanjaro, huku mshambuliaji wake Thomas Ulimwengu ndiye aliyepachia bao la ushindi.
Katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye uwanja wa Ushirika, Aman Kihata wa Kilimanjaro aliibuka mchezaji bora.
Aidha, mchezo wa pili ulizikutanisha Arusha na Tanga ambapo Arusha ilishinda mabao 3-1, huku Kibabu Chandinga wa Tanga akiibuka mchezaji bora wa mchezohuo.

Matokeo mengine:
Ilala 2-Moro 0, Tabora 2- Kigoma-1, Mbeya 2-Iringa 1, Kinondoni 0- Mtwara 1, Rukwa 2- Temeke 1, Singida 0-Kigoma 0, Pwani 2-Manyara 0.

Comments