WAREMBO 17 WACHUJWA MISS TABATA 2011


MISS TABATA 2010,CONSOLATA LUKOSI

Warembo 17 wamechujwa kwenye kinyang’ajiro cha kumsaka Miss Tabata 2011 ambayo imepangwa kufanyika mapema mwezi ujao katika ukumbi wa Da’ West Park .
Mratibu wa shindano hilo Joseph Kapinga amesema jana kuwa warembo hao wametolewa baada ya kukosa sifa ya kushiriki ikiwemo utoro na ukosefu wa nidhamu.
Waliyochujwa ni Shadya Ali (21), Consolata Michael (22), Upole Athumani (19), Chiku Adolph (18), Blandina Paul (18), Victoria Magulo (20)Irene Jafari (19), Asia Amiri (22), Catherine Geodfrey (19) na Winfrida Gilbat (21).
Wengine ni Janeth Marandu (21), Esther Simon (18), Mariam Lameck (19), Malaika Abdallah (18), Sarah Hangaya 20, Axa Sosthenes (22) na Esther Gideon (20).
“Pamoja na kuwachuja lakini bado tunaendelea kupokea warembo wenye sifa na vigezo ili ushindani uwe mkali,” Kapinga alisema.
Kapinga alisema warembo 21 wanaendelea na mazoezi katika ukumbi Da’ West Park , Tabata, chini ya wakufunzi wawili, ambao ni Rehema Uzuia 'Sweet Ray' na Joyce Joseph Kaniki.
Warembo hao ni Dorice Mutabingwa (22), Marion Augustino (19), Edina Mnada (21), Mgayo Haruna (21), Godliver Mashamba (22), Juanita Kanyika (22), Theckler Benedict (19), Lucia Joseph (20), Angela Fotnatus (20), Neema Marwa, (18) na Happiness Emmanuel (18).
Wengine ni Lucy Mboya (21), Neema Mwakibinga (21), Sweetlily Suleiman (21), Nasra Salim (21), Lilian Bryson (22), Happiness Masanja (21), Mariam Manyanya (21), Faiza Ally (19), Catherine Julius (20), Sheilah Soud (20), Augustina Mshanga (20), Cresencia Haule (20), Patricia Eliah (20) na Angela Benard (18).
Warembo 10 watapata tiketi ya kushiriki kwenye shindano la kutafuta Miss Ilala kabla ya kufuzu kushiriki kwenye Vodacom Miss Tanzania 2011.
Baadhi ya makampuni ambayo tayari wamejitokeza kudhamini Miss Tabata 2011 ni Integrated Communications, Paris Pub, Ben Expedition, Chicken Hut na Issmichuzi blogspot.
Kapinga alisema wadhamini wengine akiwemo mdhamini mkuu watatangazwa baadaye.
Consolata Lukose ndiye mrembo anayeshikilia taji la Miss Tabata. Consolata alikuwa nambari tatu mwaka jana kwenye shindano la taifa (Vodacom Miss Tanzania) kabla ya kushinda taji la Redds Ambassador.
Miss Tabata inaandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts.

Comments