WAREMBNO MISS TABATA WATEMBELEA MBUGA ZA WANYAMA MIKUMI

Na Mwandishi Wetu, Mikumi
Warembo 22 watakaoshiriki kwenye kinyang’anyiro cha kumsaka Miss Tabata 2011 jana waliondoka Dar es Salaam kwenda kutembelea mbuga za wanyama huko Mikumi.
Mratibu wa shindano hilo Joseph Kapinga alisema jana kuwa lengo la ziara hiyo ni kukuza utalii wa ndani. engo la ziara hii ni kutangaza utalii wa ndani. Tunataka warembo wetu wajue wanyama na vivutio vingine vinavyopatikana kwenye mbuga zetu hasa Mikumi,” Kapinga alisema.
Alisema kuwa wakiwa Mikumi, warembo hao wapata fursa ya kuwajua tabia za wanyama na ndege wote waliyomo kwenye mbuga hiyo.
Miss Tabata imepangwa kufanyika Juni 10 katika ukumbi wa Da’ West Park .
Warembo waliyoondoka ni Marion Augustino (19), Neema Marwa (18), Catherine Julius (20), Lilian William (20), Godliver Mashamba (22) na Dorice Mutabingwa (21).
Wengine ni Sweetlily Suleiman (21), Maria John (21), Happyness Emmanuel (18), Cresensia Haule (20), Mariam Manyanya (21), Agustina Mshanga (20), Nasra Salim (21), Faiza Ally (19) na Edina Mnada (21).
Pia wamo Angela Fortunatus (21), Lucia Joseph (20), Lilian Brayson (22), Rita Mvungi (21) na Willieth Wilson (22).
Miss Tabata 2011 inadhaminiwa na Dodoma Wine, Vodacom, Redds Original, Integrated Communications, Paris Pub, Fabak Fashion, Freditto Entertainment, Chicken Hut, Travel Partners, Ben Expedition, Screen Masters, Sean Entertainment, Screen Masters, Michuzi blogspot na Anech Stationary.
Consolata Lukosi ndiye mrembo anayeshikilia taji la Miss Tabata.
Mrembo huyo alikuwa nambari tatu mwaka jana kwenye shindano la taifa (Miss Tanzania ) kabla ya kushinda taji la Redds Ambassador.
Mashindano hayo ya urembo yanaandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts.

Comments