VODACOM YAMWAGA ZAWADI KWA WASHINDI WA LIGI KUU TANZANIA BARA

 WAZIRI WA HABARI UTAMADUNI NA MICHEZO EMMANUEL NCHIMBI AKIMKABIDHI HUNDI YA MIL.42 MJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI YA YANGA SALUM RUPIA KUTOKANA NA UBINGWA WA LIGI HIYO.
 KOCHA MKUU WA TIMU YA TAIFA YA VIJANA JAMHURI KIHWELO 'JULIO' AKIPOKEA HUNDI YA MIL.17 KWA NIABA YA KLABU YA SIMBA ILIYOSHIKA NAFASI YA PILI.
 JULIO AKIPOKEA TUZO YA MFUNGAJI BORA MRISHO NGASA WA AZAM AMBAPO PIA ALIZAWADIWA MIL.3.1
                                        ZAWADI YA TIMU ILIKWENDA KWA RUVU SHOOTING
1,2,3, ......
 
aliyekuwa kocha wa Simba, Mzambia Patrick Phiri  alitangazwa kuwa kocha bora wa msimu uliopita na kukabidhiwa hundi ya sh milioni 3.1 kutoka kwa wadhamini hao.

Aidha, mwamuzi bora wa ligi alitangazwa kuwa ni Alex Mahaji wa Mwanza aliyekabidhiwa hundi ya sh milioni 3.1, huku mchezaji wa Toto African ya Mwanza, Jacob Massawe akitangazwa kuwa mchezaji bora na kuzawadiwa sh 200,650,000 wakati timu ya Ruvu Shooting ilizawadiwa sh milioni 6.2 kwa kuwa timu yenye nidhamu.
Mabingwa wa ligi hiyo, Yanga walipewa hundi ya sh milioni 42, huku washindi wa pili Simba wakizawadiwa sh milioni 17 na Azam iliyokuwa ya tatu ikizawadiwa sh milioni 11, wakati mfungaji bora wa ligi hiyo, Mrisho Ngasa wa Azam alijitwalia sh sh milioni 3.1 na kipa wa Yanga, Yaw Berko aliondoka na hundi ya sh milioni 2.65 kwa kuwa kipa bora.

Comments