VODACOM KUWAJAZA MANOTI WASHINDI LIGI KUU BARA




Kampuni ya Vodacom Tanzania kesho inatarajiwa kukabidhi kitita cha ubingwa wa Ligi Kuu ya soka Tanzania bara kwa mabingwa wa Ligi hiyo timu ya Yanga ya Dar es salaam.


Zawadi hiyo ya fedha taslimu ni sehemu ya udhamani wa Vodacom Tanzania katika ligi hiyo inayoratibiwa na kusImamiwa na shirikisho la mpira wa miguu nchini – TFF.

Meneja Udhamini na matukio wa kampuni ya Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa amesema makabidhaino hayo yatafanyika kwenye hafla maalum ya chakula cha mchana iliyondaliwa na Vodacom na TFF kwenye Hoteli ya Paradise.

Amesema wakiwa wadhamini wakuu wa ligi hiyo ni furaha kwao kuona kwamba vipengele vya udhamini ikiwemo kipengele hicho muhimu cha zawadi ya fedha taslimu kinatekelezwa na hivyo kutoa ari zaidi ya ushindani wakati wa ligi inapochezwa.

“Ni furaha kubwa kwetu tunapoona mambo yanakwenda vizuri kwani lengo la Vodacom Tanzania ni kuona soka ikipiga hatua zaidi na hiyo ni pamoja na kuwa na ligi yenye zawadi zinazochochea ushindani na kesho bingwa Yanga atakuwa na wakati mwengine wa kufurahia kazi waliyoifanya wakati wa ligi hadi kuibuka mabingwa”Alisema Rukia

Mbali na Yanga timu nyengine zinatakazokabidhiwa zawadi za fedha taslimu ni Simba iliyomaliza ligi ikiwa nafasi ya pili na Azam FC kwa kushika nafasi ya tatu ambazo kila mmoja atakabidhiwa hundi yake katika hafla ambayo mgeni rasmi ni Waziri wa Habari,Vijana na Michezo Dk Emmanuel Nchimbi.

Kwa mujibu wa Rukia zawadi za fedha za msimu wa ligi wa mwaka 2010/2011 uliomalzia hivi karibuni zitawahusu pia wachezaji walionga’ra kwenye msimu huo akiwemo mfungaji bora,mlinda mlango bora,mwamuzi bora,kocha bora na timu iliyoongoza katika kuonyesha nidhamu.

“Simba na Azam FC nao pia kesho tutawakabidhi hundi yao lakini pia wachezaji na wadau wengine waliong’ara kwenye msimu huo wa 2010/2011 nao watakabidhiwa hundi zao zikiwa na nyongeza ikilinganishwa na zawadi za msimiu wa 2009/2010”Alisema Rukia.

Comments