VIINGILIO TAIFA STARS V BAFANA BAFANA HIVI HAPA




Mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars)
na Afrika Kusini (Bafana Bafana) itachezwa Mei 14 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 12 kamili jioni.
Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa sh. 30,000 (VIP A), sh. 20,000 (VIP B), sh. 10,000 (VIP C), sh. 7,000 (viti vya rangi ya chungwa- orange straight) na sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa (orange curve), viti vya kijani na viti vya bluu.
Bafana Bafana inatarajiwa kuwasili Mei 12 mwaka huu saa 1.30 jioni kwa ndege ya South African Airways (SAA) ikiwa na kundi la watu 30, ambapo wachezaji ni 20wakati benchi la ufundi na viongozi litakuwa na watu 10.
Stars itaingia kambini keshokutwa (Mei 7 mwaka huu) ikiwa na kikosi kile kile kilichocheza mechi ya kirafiki Aprili 23 mwaka huu jijini Maputo dhidi ya wenyeji wao (Black Mambas).

Boniface Wambura
Ofisa Habari TFF

Comments