VICKY KAMATA ALA SHAVU LA KUREKODI NA KUNDI LA MUZIKI NCHINI UINGEREZA

MBUNGE wa Viti Maalum, Victoria Kamata, ambaye pia ni mwimbaji wa muziki wa Kizazi Kipya ‘Bongo Flava’ ameingia mkataba wa miaka mitano na kundi la muziki la West coast Universal la nchini Uingereza.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamata alisema kuwa katika mkataba huo atakuwa akishiriki kuimba nyimbo ambazo ametungiwa na sio alizotunga mwenyewe.
Kamata alisema, katika hatua ambayo amefikia ni miujiza kwake kutokana na kundi hilo kumuona anafaa, kwani linatambulika kimataifa katika muziki.
Alisema, mkataba huo ameingia mwanzoni mwa Machi mwaka huu na kushiriki katika wimbo mmoja ambao unakwenda kwa jina ‘Right it Up’.
Kamata alisema kuwa, wimbo huo utaingia sokoni baada ya kutengeneza video ambapo ametakiwa kupungua kilo 10 ili aweze kwenda sambamba na miili ya magwiji hao wa muziki.

Comments