U-23 v NIGERIA KUKWAANA USIKU WA JUNI 5 UWANJA WA TAIFA


Mechi ya kwanza ya mchujo ya michuano ya Olimpiki kati ya timu ya Taifa ya Tanzania kwa vijana wenye umri chini ya miaka 23 dhidi ya Nigeria itachezwa Juni 5 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 1 kamili usiku.
Tumepanga muda huo kwa vile uwanja siku hiyo utakuwa unatumika kwa ajili ya michuano ya riadha ya Kanda ya Tano Afrika ambapo itakuwa inafikia kilele.
Kwa mujibu wa Chama cha Riadha Tanzania (AT) kufikia saa 8 mchana michuano hiyo itakuwa imemalizika, hivyo kupisha maandalizi ya mechi.
Mechi itachezeshwa na mwamuzi Sylvester Kirwa ambapo atasaidiwa na Peter Kiereini, Aden Marwa na Davies Omweno wote kutoka Kenya wakati Kamishna wa mchezo huo atakuwa Sahilu Gebremariam kutoka Ethiopia.

Boniface Wambura
Ofisa Habari TFF

Comments