TASWA KUENDESHA MJADALA KWA WADAU WA MICHEZO, WAANDISHI KUPIGWA MSASA


CHAMA cha Waaandishi wa Habari za Michezo (TASWA), kinatarajia kuendesha mjadala wa wazi kwa wadau wa michezo mbalimbali Julai 16 mwaka huu jijini Dar es Salaam ili kuweza kukusanya mawazo yao na kuyafikisha kwa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo
Katibu Mkuu wa Taswa Amir Mhando (pichani kushoto) anmesema leo kwamba mjadala huo ni muhimu katika mustakabali wa michezo nchini ili kupata mawazo ya wadau mbalimbali kabla ya kuyafikisha kwa chombo husika na kuweza kufanyiwa kazi.
Alisema kuwa mjadala huo utashirikisha vyama mbalimbali vya michezo makampuni, mashirika, wadau na taasisi nyingine.
Aidha, Taswa inatarajiwa kuwapiga msasa waandishi wa habari za michezo nchini mwezi Septemba itakayofanyika katika miji ya Morogoro na Arusha ambapo alisema ile ya Morogoro itafanyika  Septemba 18-24 na kushirikisha waandishi toka mikoa ya Pwani, Lindi, Mtwara na Dar es Salaam, huku ile ya Arusha itafanyika Septemba 23-29.
Amir aliongeza kuwa semina nyingine inatarajiwa kufanyika Septemba 26-27 na kuhusisha waandishi waandamizi na wahariri wa michezo ambayo itafanyika Bagamoyo.

Comments

  1. ningependa kuuliza ile mechi waliyoitangaza TASWA baina ya bingwa wa ligi dhidi ya wachezaji waliongara katika ligi (all vodacom stars) inachezwa lini, kama teyari nani aliibuka mshindi, au imefutwa. Natumai utanisaidia kwa hilo
    www.aboodmsuni.blogspot.com

    ReplyDelete

Post a Comment