TAMASHA LA MTEMI MILAMBO KURINDIMA JULAI 8-10 UWANJA WA CHIPUKIZI, TABORA

NA MWANDISHI WETU

TAMASHA la ngoma za utamaduni na maonyesho ya biashara la Mtemi Milambo linatarajiwa kufanyika Julai 8 hadi 10 katika Uwanja wa Chipukizi mjini Tabora ambapo litawezesha kukuza mila na utamaduni kwa makabila ya Tanzania hususani makabila makubwa ya mkoa huo na jirani ya Wanyanwezi na Wasukuma.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Taasisi ya Chief Promotions, Amon Mkoga ambao ndio wandaaji wakuu wa tamasha hilo, alisema kuwa tamasha hilo litakuwa ni la aina yake kwa mwaka huu na litasaidia kuenzi na kuendeleza utamaduni wa Mtanzani, hususani makabila makubwa ya mkoa ya Tabora,Shinyanga na Mwanza ambapo makabila makubwa ya Wasukuma na Wanyamwezi ambapo wataonyesha bidhaa mbalimbali zenye asili ya kitanzania sambamba na michezo ya asili ikiwemo mchezo wa bao na kurusha mishale.
Mkoga alisema kuwa shughuli za tamasha hilo zinatarajia kuanza asubuhi ya saa nne hadi saa 12 jioni kuanzia Julai 8 hadi Jumapili ya Julai 10, ambapo wakati wote huo, ngoma mbalimbali za zitatumbuiza na kuonyesha utamaduni wake. “Ngoma zitakazotumbuiza kuwa ni pamoja na Manyanga, Maswezi, Uyeye, Bagalu, Bagika, Bagika, Bazuba, Radu na nyingine nyingi hivyo tunaomba kufika kwa wingi ilikujionea sambamba na kuwaunga mkono katika bidhaa zao” alisema Mkoga.
Naye, Meneja wa bia ya Balimi miongoni mwa wadhamini wa tamasha hilo, Edith Bebwa alisema kuwa, wamejitokeza kudhaamini kwa mara ya pili mwaka huu ili kuwaenzi wateja wao hao ambao bia hiyo ni mahususi kwa wakzi wa kanda ya Ziwa. “Ngoma hizi za wasukuma na wanyamwezi huchezwa sana wakati wa mavuno, hivyo kwa kuwa Balimi ni bia ya mkulima tumeona tuungane kusherekea pamoja wakati wa mavuno huku huku tukienzi utamaduni wa Kitanzania” alisema Bebwa.
Aidha, katika tamasha hilo , mgeni rasmi anatarajia kuwa mkuu wa mkoa wa Tabora, Abeid Mwinyimusa, ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘Kushoke kukaya’ yaani turudi nyumbani tafsiri ya Kiswahili toka kinyamwezi.
Mbali na kampuni ya bia Tanzania (TBL), kupitia bia yake ya Balimi, wadhamini wengine ni Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Ubalozi wa Switzerland , Kalunde

Comments