SIMBA YAWALETA BIRMINGHAM FC

MABINGWA wa Carling Cup timu ya soka ya Birmingham ya nchini Uingereza itatua nchini mwezi Julai kwa ziara ya kimichezo.
Mwenyekiti wa Simba ambao watakuwa wenyeji wa timu hiyo hapa nchini Alhaj Ismail Aden Rage (Pichani kushoto), amesema leo kwamba timu hiyo itakipiga na Simba Julai 7, kabla ya kukipiga na Yanga Julai 12, mechi zote zitachezwa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Alisema maofisa wa timu akiwemo kocha msaidizi Andy Watson na daktari Ian Mc Guinness watawasili nchini Mei 9 kwa ajili ya kukagua uwanja na hoteli ya Kilimanjaro Kempisk kuona kama vinakidhi viwango vya timu yao.
Aidha, timu hiyo itakuja na mashabiki 1000 ambao watajigharamia malazi pamoja na gharama byingine zikiwemo za uwanjani.

Comments