SIMBA WAENDA KUSAKA MAKALI TANGA



KATIKA kujiandaa na mechi yake ya kombe la Shirikisho dhidi ya DC Motema Pembe ya DRC, timu ya Soka ya Simba inatarajiwa kwenda mkoani Tanga kwa ajili ya kufanya maandalizi yake.



Simba ilianza kujifua jana katika viwanja vya TCC Chang'ombe huku safari ya kwenda Tanga ikitarajiwa kuwa kesho.


Wachezaji wa Simba wameapa kumaliza hasira zao za kutolewa kwenye ligi ya mabingwa Afrika kupitia Wacongo hao.

Simba ilifungwa mabao 3-0 na Wydad Casablanca.

Comments