SIMBA v WYDAD CASAMBLANCA KUKWAANA MEI 27,28 AU 29


Mechi ya kutafuta nafasi ya kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) kuondolewa kwa kuchezesha mchezaji asiyestahili imepangwa kufanyika kati ya Mei 27, 28 na 29 mwaka huu kwenye uwanja huru (neutral ground).
Simba ya Tanzania na Wydad de Casablanca ya Morocco ndizo zitakazopambana katika mechi hiyo ya mkondo mmoja. Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) linatarajia kutaja katika muda mfupi ujao nchi ambapo mechi hiyo itachezwa.
Timu itakayoshinda itaingia katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa, ikiwa kundi B pamoja na Al Ahly ya Misri, Esperence (Tunisia) na Moloudia Club d’Alger ya Algeria. Timu itakayoshindwa itaingia katika hatua ya 16 bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho ambapo itacheza mechi ya kwanza nyumbani na Daring Club Motema Pembe ya DRC kati ya Juni 10, 11 na 12 mwaka huu.

Comments