SHEIKH YAHAYA HUSSEIN AFARIKI DUNIA

MNAJIMU mkuu na bingwa wa kuhifadhi Qur-an Afrika Mashariki na Kati, Sheikh Yahaya Hussin amefariki dunia leo asubuhi.
Taarifa za kifo chake zilizothibitishwa na Muft wa Tanzania Sheikh Issa Bin Shaaban Simba zinasema kuwa marehemu Sheikh Yahaya alikutwa na umauti huo katika hospitali moja na baada ya kuwa katika maradhi ya kawaida yatokanayo na utu uzima aliokuwa nao.
Muft Simba alisema BAKWATA imepokea kwa masikitiko kifo cha Sheikh Yahaya na kuwaomba Watananzia wamuiombee ili akapumzike kwa amani.
Mazishi ya yake yanatarajiwa kufanyika kesho kwani familia ipo katika taratibu za mipango hiyo.
INNALILAH WAINNA ILAIH RAJUUN

Comments