SAMATTA, OCHAN SI MALI HALALI YA SIMBA TENA- CAF YASISITIZA

                                                                                 PATRICK OCHAN
                                                                                     MBWANA SAMATTA
Wachezaji Mbwana Samata na Patrick Ochan ambao Simba inataka kuwatumia kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco hawana uhalali wa kuchezea timu hiyo.
Simba kupitia TFF ilitaka kufahamu kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kama inaweza kuwatumia wachezaji hao kwa vile Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kuichezea TP Mazembe bado haijatolewa.
Kwa mujibu wa CAF, hawawezi kuichezea Simba kwa vile tayari wameuzwa, hivyo kutokuwa na sifa ya kuwa wachezaji wa timu hiyo kwa mujibu wa Ibara ya 26(1) ya Kanuni za Ligi ya Mabingwa Afrika.
Sifa ya mchezaji kwa mujibu wa kanuni hiyo ni kuwa na leseni iliyotolewa na chama cha mpira wa miguu cha nchi yake, leseni ya CAF, awe anaichezea timu inayoshiriki Ligi ya Mabingwa kwenye ligi ya nchi husika na awe anaishi katika
nchi ilipo timu anayoichezea.

Boniface Wambura
Ofisa Habari TFF

Comments