SACODEA YAJIVUA GAMBA KWA POLISI IRINGA

TAASISI ya Southern Corridor  Development Association (SACODEA) ya mjini Iringa  imeamua kuirudisha timu ya soka ya  Polisi Iringa kwa jeshi la polisi kutokana na sababu mbalimbali na kutopata ushirikiano wa kutosha toka Chama cha Soka mkoa wa Iringi (IRFA).
 Kwa mujibu wa barua ya mwenyekiti wa Sacodea, Fredrick Mwakalebela kwenda kwa Mkuu wa Pilisi Wilaya ya Iringa ya  Iringa wamefikia maamuzi hayo baada ya kuambiwa na IRFA kuwa timu hiyo haitambuliwi mahala popote,jina la Polisi Iringa halitabadilishwa mpaka baada ya miaka kadhaa sababu utaratibu kama huo haupo.
Barua hiyo hiyo iliongeza kuwa sababu nyingine ni kuwa timu ya Polisi haiwezi kupewa kwa wababaishaji kama Sacodea na pia hairuhusiwi kucheza mechi yoyote hata iwe ya kirafiki.
Barua hiyo ilieleza kuwa, awali utaratibu wa kuandaa katiba ya timu mpya ambayo ilikuwa iitwe IRINGA  FOOTBAL CLUB ulikamilika,  na Afisa Utamaduni wa Wila yaIringa Mjini alipitisha katiba na Chama Cha Soka cha Wilaya kilitusaidia sana kupitisha a hatimaye kwenda  kwa msajili wa vyamavya michezo Taifa  ambaye aliwashauri  TFF wakaipitie .
“TFF nao waliipitisha na kutushauri tuipeleke  ngazi ya  Mkoa lakini cha kusikitisha ndipo tukakumbana na hali kama hiyo hivyo hatuna budi kuirudisha timu hiyo katika miliki yenu”, Aliongeza Mwakalebela katika barua yake.
 “Tulishukuru sana tulipopokea barua yako ya tarehe  26/02/2011 yenye kumbukummbu No IR/A.23/3/VOL. 111/305 uliyomuandikia katibu  wa chama cha Soko wilaya ya Iringa nakala kwa katibu wa  Soka wa mkoa wa Iringa na SOCODEA kupata nakala”, ilisema sehemu ya barua hiyo .
“Kitendo cha kukabidhiwa timu kwenye shirika kilileta hamasa kubwa sana kwa wana Iringa hasa kufahamu fika kuwa timu itacheza ligi  kuu ya Tanzania bara baada ya kupata wafadhili wa kudumu”.

Comments