MWANZA HEROES YAITA MASHABIKI FAINALI KILI TAIFA CUP

KOCHA MSAIDIZI WA MWANZA HEROES JOHN  TEGETE NA MWANAYE JOHN TEGETE ANAYEKIPIGA KATIKA TIMU HIYO 
SIKU moja tu baada ya kukata tiketi ya kucheza fainali ya mashinado ya Kili Taifa Cup 2011, kocha msaidizi wa timu ya Mwanza, John Tegete, amewataka wapenzi wa mkoa wa Mwanza kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao.

Akizungumza mjini hapa jana, kocha huyo alisema ana imani kubwa na kikosi chake na wana uhakika mkubwa wa kunyanyua kombe.
Mechi ya fainali inatarajiwa kupigwa siku ya Jumamosi katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Mjini Arusha.
Tegete alisema kikosi chake kitacheza kufa na kupona ili kiweze kunyakuwa ubingwa huo.
"Nadhani kila mtu anatambua kama tumeingia fainali tunasubiri timu yoyote kati ya Kagera au Mbeya ili tucheze nayo sisi wala hatuna wasiwasi ubingwa tunachukua kikubwa tunaomba wanamwanza wajitokeze kutushangilia mwanzo hadi mwisho,"alisema Tegete Baba mzazi wa mchezaji wa timu hiyo Jerryson Tegete.
Mwanza ilipata nafasi ya kutinga fainali baada ya kuwafunga Ilala ya Dar es Salaam, juzi kwenye Uwanja wa Shehk Amri Abed Arusha.
Mchezaji Jerryson Tegete alichangia kwa kiasi kikubwa kuifikisha timu yake katika fainali hizi baaday ya kufunga mabao mawili na pia kutangazwa mchezaji bora. Alizawadiwa shilingi laki moja kwa hisani ya Kilimanjaro Premium Lager.
Kocha wa Mwanza alisema maandalizi ya mchezo huo yanaendelea vizuri na kwamza wachezaji wake wana ari kubwa ya kuibuka na ushindi huo.
Mechi ya kumpata mshindi wa tatu inatarajiwa kuchezwa kesho Ijumaa kabla ya fainali ya Jumamosi. Leo timu zote zinapumzika ili kujiandaa na mechi ya kesho na fainali.
Mashindano haya yamedhaminiwa na Kamuni ya Bia Tanzania kupitia kinywaji chake cha Kilimanjao Premium Lager na masual aya habari kuratibiwa na kampuni ya Executive Solutions.

Comments