MSEMAJI WA SIMBA CLIFFORD NDIMBO AJIVUA GAMBA

MSEMAJI wa klabu ya soka ya Simba, Clifford Ndimbo ameamua kujiuzulu rasmi wadhifa wake huo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kutopata ushirikiano wa kutosha baina yake na baadhi ya viongozi wa klabu hiyo.
Ndimbo amesema kwamba kama msemaji wa klabu hiyo ameshindwa kutimiza wajibu wake ipasavyo kutokana na 'siasa' za klabu hiyo hivyo ameona ajiweke kando na kuendelea na mambo mengine.

Comments