MECHI YA STARS,BAFANA BAFANA YAINGIZA MIL.75

Pambano la kirafiki kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Afrika Kusini (Bafana Bafana) lililochezwa Mei 14 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh. 75,888,000 kutokana na watazamaji 10,554 walionunua tiketi. Watazamaji 240 walilipa sh. 30,000, 585 (sh. 20,000) na 1,423 (sh. 10,000), 614 (sh. 7,000) na 7,692 (sh. 5,000).
Baada ya kuondoa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 11,576,135.59 na gharama za awali za mchezo ambazo ni sh. 21,843,600.00 mgawo ulikuwa kama ifuatavyo; asilimia 10 kwa uwanja sh. 4,246,826.44, asilimia 10 kwa gharama za mchezo sh. 4,246,826.44, asilimia 5 kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 2,123,413.22 na asilimia 75 kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 31,851,198.31.
Nacho Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) kilipata asilimia tano kutoka kwa mgawo wa TFF ambayo ni sh. 1,592,559.92.

SEMINA YA WAAMUZI WA FIFA
Semina kwa waamuzi wanaotambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) itafanyika Dar es Salaam kuanzia Mei 17 hadi 19 mwaka huu. Wakufunzi wa semina hiyo ni Riziki Majalla, Leslie Liunda na Omari Kasinde.
Waamuzi hao ni Ramadhan Ibada, Waziri Sheha, Oden Mbaga, Judith Gamba na Israel Mujuni. Waamuzi wasaidizi ni Hamis Chang’walu, Ally Kombo, Saada Tibabimale, Josephat Bulali, Samuel Mpenzu, Erasmo Jesse, Mwanahija Makame, John Kanyenye na Khamis Maswa.
Boniface Wambura

Ofisa Habari TFF

Comments