MCHEKESHAJI AYOUB SANTANA ANAKUJA KIVINGINE

MCHEKESHAJI anayefanya vema katika medani hiyo Ayoub Santana (Pichani Kushoto) yupo mbioni kuingiza sokoni kazi zake.
Santana amesema kwamba kazi hizo ni za kwanza kuziandaa kwa mkono wake ambapo ndani yake atawashirikisha wachekeshaji kadhaa.
Kwa wanaofuatilia filamu za kibongo wameshaona kipaji cha Santana kupitia filamu kama Money Desire,Its Too late,Fake Pregnant,Kisisina,Where is Love, Aunt Suzzy,No way Out, The Romantic, More than Crazy, Mahoka, penzi la Teja, Umekasirika, Ladies Angels na nyinginezo.

Comments