MBWANA MATUMLA ATWAA UBINGWA WA MABARA

MBWANA MATUMLA

BONDIA Mbwana Matumla jana alifanikiwa kutwaa ubingwa wa mabara unaotambuliwa na chama cha UBO baada ya kumshinda kwa pointi Mkenya Gabriel Ochieng katika uzito wa Bantam.

Katika pambano hilo la raundi 12 lililofanyika kwenye ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es Salaam, Ochieng alijikuta akiangushwa katika raundi ya 11, huku pambano hilo ambalo mwamuzi wake alikuwa Anthony Ruta, jaji Billy Kiremi alitoa pointi 120 – 117 ,huku jaji Hassan Mwingira alitoa pointi 120 – 114 na Jalus Ligongo alimpa Matumla pointi 116 - 113.

Comments

Post a Comment