MATOPE,MADIMBWI YA MAJI YAPUNGUZA KASI YA MECHI KATIKA UWANJA WA USHIRIKA, MOSHI




























MCHEZAJI BORA WA MECHI BAINA YA TIMU YA VIJANA CHINI YA MIAKA 23 V ARUSHA, GODFREY WAMBURA AKIPOKEA ZAWADI YA SHULINGI 100,000.


MVUA zilizonyesha mjini Moshi usiku wa kuamkoa jumatano ziliupelekea uwanja wa Ushirika kujaa maji na matope hivyo kupelekea wachezaji wa timu za U-23, Arusha, Tanga na Kilimanjaro mkushindwa kujiachia ipasavyo waliposhuka dimbani katika mzunguko wa mwisho wa hatua ya awali ya michuano ya Kili Taifa Cup.

Hali hiyo iliwafanya wachezaji kucheza kwa kujihamia hasa ikizingatiwa hali ile iliwafanya wateleze hivyo walikuwa makini katika usalama wao zaiudi.Pamoja na hali hiyo timu zote zilionyesha kandanda safi huku katika mechi baina ya Arusha na U-23 zilikwenda sare ya bao1-1, huku Tanga ikiifunga Kilimanajaro bao 1-0.

Kwa mantiki hiyo kituo cha Kilimanjaro kimetoa timu mbili kwenda hatua ya robo fainali, Arusha na U-23.

Comments