MATAKA AJIVUA GAMBA ATCL

MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania (ATC), David Mataka (60) ametangaza kustaafu.
Mataka alitangaza hatua yake hiyo katika ukumbi wa mikutano wa ATC mbele ya waandishi wa habari huku akimtupia lawama Rais mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa kwa kumsimamisha kazi kipindi cha utawala wake.
Mataka alikumbwa na kadhia hiyo wakati wa utawala wa Mkapa alipokuwa mfanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PPF) na kumsimamisha kazi  ili kupisha uchunguzi kutokana na kashfa ambazo zilikuwa na lengo la kumchafulia jina.
"Sijafukuzwa kazi ila nimestaafu kutokana na umri wangu kisheria kunitaka nifanye hivyo.....Nimezaliwa May  11 ,  1951 , hivyo tayari nimetimiza  miaka 60", Alisema.

Comments