MAPRO WA TZ KUJA KUWANOLEA MAKALI CAR

                                                                NIZAR KHALFAN
                                                     HENRY JOSEPH
IDRISSA RAJAB

                                                                      ABDI KASSIM
                                                                   MBWANA SAMATTA
                                                        ATHUMAN MACHUPPA
DANNY MRWANDA
NYOTA wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ wanaocheza soka ya kulipwa wanatarajia kuanza kutua leo jijini Dar es Salaam kwa mafungu ili kujiunga na wenzao ambao wapo kambini kujiandaa na mchezo wa kusaka tiketi yake ya kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika dhidi ya Jamhuri ya Afrika Kati ulipangwa kupigwa Juni 5 mwaka huu jijini Bangui.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Angetile Osiah, amesema kuwa mshambuliaji anayekipiga katika klabu ya Tp Mazembe ya Congo, Mbwana Samatta ndiye atakayefungua dimba.
Alisema wachezaji wengine wote wamethibitisha kuja  kujiunga na wenzao  ambao wapo kambini chini ya kocha mkuu Jan Poulsen.
Aliwataja wachezaji hao kuwa ni pamoja na Idrisa Rajab,  Athumani Machupa, Nizar Khalfani, Abdi Kassim, Danny Mrwanda na Henry Joseph.

Comments